Ntaweka picha nkipenda….
Nkipenda ndio ntaweka picha
Sitawaficha nimpendae ju najuwa yeye ni maua
Sabuni ya moyo wangu
uso wangu utauona uking’aa ishara tosha…kuwa nlimpata kipenzi cha moyo wangu
So…nkipenda ntaweka picha
Ntaweka picha ya bwana ampendaye bibi,kijana hatamani mabinti…picha ya kumpenda in a thousand ways
Ntaweka picha ya bibi na bwana
Kwa mapenzi yenye hawaezi achana aty juu hawana…wana
Ntaweka picha ya bwana kumpeleka bibi out…ndani ya nyumba…kumpikia wali,, samaki na uji Wa wimbi…picha ya bibi akifurahi
Ntaweka picha ya bwana akimwosha bibi…miguu
Picha ya furaha bwana akimbeba bibi…juu juu
Ntaweka picha ya baba na bwana ya bibi
Picha ya wana wakicheza hukunkimtunza wangu msiri
Ntaweka picha ya bibi akiwa mzito
Picha ya bwana akipika akimlisha chakula kizito
Na akifuwa nguo za wana na kutayarisha mapito
Ntaweka picha ya bwana anayesema,bibi anaambilika
Picha tukijadili majukumu na tukiwajibika
Ntaweka picha bibi na mama
Picha akitunza bwana na akitunza wana
Akiwalisha na wakicheza mchana
Ntaweka picha waone…
Nataka waone jinsi ya kupenda
Kutunza,,kusema na kutenda
Nataka waone jinsi ya kupenda bibi
Kumchunga na kumlinda msiri kwa bidii
Nataka waone mapenzi ya dhati…waone tukila mahindi choma na bado tunapendana
Nataka kuona wakipenda na kupendana nasi mapenzi ya peremende
#picha
#mwas
Awesome piece!
Thanks