Nilikupenda tangu…
nakumbuka hadi mamangu akikwambia aty utakuwa wangu…
Wangu wakupenda
Wangu msiri kwa yote tungeyatenda
Wangu kulisha na wangu kunilisha
Wangu wakuenzi masiku na miezi
Wangu….
Nilikupenda
Nilikupenda siku zenye hukuwa unajuwa love ni nini?!…siku zenye love kwako ilikuwa tabiya mbaya…tukitembea na wewe hizo siku ulikuwa unaskia haya
Nilikupenda ukiwa mweusi…time nlikuwa na chora giza,,nai-cut out na kuipaint white….time sikuwa na kitu BT nilikuwa na kiti moja ya mbao yenye ulipenda sana kukalia,,,ukilala nlikuwa na kulaza kwa matress yangu yenye ilikuwa chini
Izo time nilikuwa down BT ulikuwa unaniamini
Nilikupenda time hakukuwa na simu…time kuongea na wewe iliwanga barua
Barua zenye tungetuma secretly ju mama angeraruwa
Nlikupenda time singeafford kununuwa maua…time yenye ningechuna maua kwa njia
Nkuletee usiku na nijichunge your dad juu angeniua
Nlikupenda time singeafford sukari…time yenye chakula ilikuwa supper
Ugali na maji nikibarikiwa naiongezea ladha ya chumvi
Nlikupenda time kutravel ilikuwa ya msimu….time ningetaka kusafiri ilikiwa headache juu ningefaa ku-book baisikeli ya jirani mapema
Juu hiyo baisikeli ilikuwa inapelekwa service asubuhi na mapema yenye ungekam jioni hangekusaidika
jirani alikuwa na msemo wake Wa…”siungesema mapema”
Nilikupenda time hukuwa unajuwa kupika…time yenye nlikuwa napika Kila kitu wewe unapika chai
Nlikupenda time hukuwa unajuwa kuoga vizuri…time yenye singekulaumu sana juu kulikuwa na shida ya maji
Nlikupenda time ulikuwa unashema …time yenye the only language ulijuwa ilikuwa lugha ya mama
Siku mind kukuskia ukikosea…juu sauti yako ilikuwa inani-drive crazy
Nilikupenda….
Nilikuwa na kupenda…
Nakupenda mpaka Wa Leo na singependa…tukitengana
Wewe ni bibi na mama ya Watoto wangu singetamani tukiachana
Nlikupenda Jana…Leo nakupenda zaidi
Jana nlikununulia gari Leo nakuahidia meli
Jana nlikununulia lesso Leo nakuahidia kitengeJana tulikula ugali kwa mboga Leo tutaila kwa nyama
Mama…sasa ni miaka kumi
Nipende nikupende zaidi
Tupange ya kesho ndio tuenzi mapenzi yetu
By Mwas
Email: hramwash@gmail.com